BOIPLUS SPORTS BLOG

MLINZI wa kushoto wa Simba Mohamed Hussein 'Tshabalala' ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa timu hiyo kwa mwezi Oktoba baada ya kuwazidi mastaa wenzake kwa kupata kura nyingi zaidi.

Tshabalala anayesifika kwa nidhamu na kujituma mazoezini na kwenye mechi, amekuwa mhimili mkuu wa ulinzi kwa upande wa kushoto tangu aliposajiliwa na kumpoteza kabisa Issa Rashidqqq 'Baba Ubaya' ambaye baadaye alirejea Mtibwa.

Kwa kutwaa tuzo hiyo, Tshabalala amejinyakulia kitita cha sh 500,000 inayotolewa na uongozi wa timu hiyo kama motisha kwa wachezaji wanaofanya vizuri.

Simba ipo jijini Mwanza inakojiandaa na mchezo dhidi ya Mwadui utakaochezwa siku ya jumamosi mjini Shinyanga.

Post a Comment

 
Top