BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
TIMU ya Taifa ya Uganda 'The Cranes' imetawazwa mabingwa wa michuano ya 14 ya CECAFA  maarufu kama Kombe la Chalenji  baada ya kuifunga Rwanda bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa leo jijini Adis Ababa Ethiopia.


Picha kwa hisani ya Kawowo.com

Cranes walifanikiwa kupata bao hilo pekee katika mchezo huo uliokuwa mgumu na wa vuta nikuvute katika dakika ya 14 kupitia kwa Ceasar Okhuti akiunganisha kwa kichwa krosi ya Dennis Okot.

Vijana hao wa kocha Milutin Micho walionyesha uwezo mkubwa na kustahili ubingwa wa michuano hiyo iliyomalizika rasmi leo.

Katika mchezo wa awali wa kutafuta mshindi wa tatu, ambao uliwakutanisha wenyeji Ethiopia dhidi ya Sudan, Ethiopia waliibuka washindi kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya kumaliza dakika 90 wakitoka sare ya bao 1-1.

Post a Comment

 
Top