BOIPLUS SPORTS BLOG

Madrid, Hispania
KAMPUNI ya ndege ya Emirates ambayo ni wadhamini wa Real Madrid, imetoa ndege mpya ambayo imepambwa kwa picha za mastaa wa timu hiyo.


Ndege hiyo A380 ambayo itakuwa ikisafiri katika vituo 36 duniani itaendelea kuruka ikiwa imepambwa kwa picha hizo kwa muda wa miezi sita.

Mastaa wanaoonekana katika kuta za ndege hiyo ni Christiano Ronaldo, Gareth Bale, Sergio Ramos, James Rodrigues, Karim Benzema na Marcelo.


Hii hapa ni video inayoonyesha upambaji hadi mastaa hao walipoenda kuitazama.

videoPost a Comment

 
Top