BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
KLABU bingwa ya Afrika, TP Mazembe leo imeondolewa kwenye michuano ya kusaka klabu bingwa ya Dunia inayoendelea nchini Japan, baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Sanfrecce Hiroshima. Mchezo huo umepigwa jijini Osaka.

Mshambuliaji wa Hiroshima,  Tsukasa Shiotani aliipatia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 44 akiunganisha kona iliyongwa kutokea upande wa kulia.Mazembe ambao walitawala mchezo katika kipindi cha kwanza walishindwa kuzitumia vema nafasi walizopata licha ya kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Hiroshima.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wajapani wakionyesha kujiamini zaidi na kuanza kuliandama lango la Mazembe. Mashambulizi hayo yalizaa matunda baada ya kupata kona iliyounganishwa kwa kichwa na Hisato Sato na kuipatia Hiroshima bao la pili katika dakika 56.Jahazi la Mazembe lilizamishwa kabisa na Takuma Asano aliyeingia kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao la pili, Sato. Asano alifunga kwa kichwa katika dakika 78 na kuufanya ubao wa matokeo usomeke 3-0 hadi mwisho wa mchezo huo.

Post a Comment

 
Top