BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi 'Mido', Zanzibar
SIMBA wanajiamini mno. Leo baada ya mazoezi yake ya asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Amaan uliopo visiwani Zanzibar wameweka wazi kuwa wameiva na wapo tayari kuwakabili Azam Fc katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa Desemba 12, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kimtazamo wadau wa soka wanajua kwamba Simba wanaweza kufungwa na Azam lakini jambo hilo wamekataa katakata kuwa hafungwi mtu siku hiyo bali watawapunguza kasi wapinzani wao ambao wapo kileleni kwa pointi 25.Meneja wa Simba, Abbas Ally ameiambia BOIPLUS ambayo imepiga kambi visiwani humo kufuatilia maandalizi ya Wekundu hao wa Msimbasi kuwa kila mchezaji ana ari na morali kubwa ya mchezo huo hivyo wanachosubiri ni kuingia uwanjani na kuchukuwa pointi tatu.

Utamu wa Simba sasa umeongezeka baada ya kurejea kwa mshambuliaji wao Mkenya, Raphael Kiongera ambaye wanachama na mashabiki wa timu hiyo wanamkubali kwa kiwango chake tangu asajiliwe na Simba japokuwa msimu uliopita hakuichezea timu hiyo kutokana na kuwa majeruhi.

Wachezaji waliokuwa na timu ya taifa ya Kilimanjaro Stars walijiunga na kikosi hicho jana jioni huku Juuko Murshid ndiye mchezaji pekee ambaye bado hajajiunga na kikosi hicho kwani alikuwa na timu yake ya taifa ya Uganda iliyotwaa ubingwa wa Kombe la Challenji.

Viungo Jonas Mkude na Awadhi Juma wao wamepewa mapumziko na daktari wa timu hiyo Yassin Gembe ambao wanasumbuliwa na malaria.

''Timu iko vizuri kama inavyoonekana wachezaji wana ari hivyo tunasubiri muda ufike tuingie uwanjani,'' alisema AbbasKivutio kikubwa katika mazoezi ya leo ilikuwa ni Hija Ugando na Kiongera ambao wanafanana na kuwa kama mapacha kwa kila kitu ikiwemo nywele zao ambazo wamefuga na kuziacha ndefu na kitengenza 'staili' ya Afro.

Simba pia imempandisha mshambuliaji wao Alex Masawe ambaye usajili wake ni wa U-20 ili kuimarisha kikosi cha hasa safu ya ushambuliaji.

Post a Comment

 
Top