BOIPLUS SPORTS BLOG

London, Uingereza
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anafikiria kutafuta mshambuliaji atakayempa changamoto Olivier Giroud na jina la straika aliye kwenye kiwango bora kabisa huko nchini Ujerumani, Javier Hernandez 'Chicharito' ndilo linalotawala kwa sasa.


Kwa mujibu wa SPORT, washika bunduki hao wameandaa ofa ya kitita cha Euro 18 milioni kwa raia huyo wa Mexico ambaye ni tegemeo katika kikosi chake cha Bayer Leverkusen.

Chicharito ambaye hakuwa kwenye mipango ya Luis Van Gaal ndani ya Manchester United, ameshaifungia Leverkusen mabao 19 katika michezo 22 tu aliyoichezea msimu huu ambayo ni mengi kuliko idadi ya mabao yaliyofungwa na wachezaji wote wa Man United msimu huu.

Arsenal pia wanatajwa kutaka kumsajili kiungo wa ulinzi baada ya Francis Coquelin kuwa majeruhi. Viungo wanaotazamwa zaidi ni Mohamed Elneny wa FC Basel na Danilo Pereira wa Porto.

Post a Comment

 
Top