BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KATIKA kile kinachooneka kuwa maisha ya kiungo wa Yanga raia wa Brazil, Andrey Coutinho, ndani ya klabu hiyo ni mafupi, Yanga ipo kwenye mchakato wa kumleta nchini kiungo Issoufou Boubacar Garba raia wa Niger atakayechukuwa nafasi yake.Ingawa haijatangazwa rasmi, BOIPLUS inajua kuwa mkataba wa Coutinho utasitishwa mara moja endapo tu kiungo huyo anayetumia zaidi guu lake la kushoto atafuzu majaribio yake ambayo yataanza mara atakapotua nchini.

Garba ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Diego, ametumia miaka yake mingi akicheza soka nchini Tunisia katika klabu maarufu ya Club Africain lakini pia akiwa amewahi kuitumikia ASFAN ya nchini kwake Niger kabla hajarudi Tunisia kuichezea Jeunesse Sportive ambayo amemalizanayo mkataba.

Yanga inahaha kutafuta wachezaji wenye hadhi ya Klabu Bingwa Afrika na sasa wanatumia mawakala mbalimbali kuwasaidia kupata wachezaji hao.

Post a Comment

 
Top