BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
YANGA ilikamilisha usajili wake wa dirisha dogo dakika za mwisho mwisho kwa kuwapa mikataba wachezaji wao Paul Nonga na  Mniger, Issofou Boubacar kutoka nchini Niger,  sasa wameamua kumleta Jerome Sina aliyekuwa akiichezea Rayon Sports ya Rwanda.

Jerome SinaYanga wanaonekana kutaka kujiimarisha zaidi kwenye Ligi Kuu Bara na hata michuano ya kimataifa ambapo wanajiandaa na michuano ya Mabingwa wa Afrika na tayari kiungo huyo alianza mazoezi yake leo asubuhi yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani.

Jerome atakuwepo na Yanga kwa majaribio ya siku kadhaa lakini hata kama watamuhitaji itakuwa si kwa ajili ya ligi kwani tayari Yanga imetimiza idadi ya wachezaji saba wa kigeni ingawa wamemsimamisha kiungo wao Haruna Niyonzima kwa muda usiojulikana.Baada ya mazoezi hayo, mchezaji huyo aligoma kuzungumza jambo lolote na mmoja wa viongozi wa Yanga walisema kuwa Jerome amekuja kwa ajili ya majaribio na si vinginevyo kwani hata dirisha la usajili limefungwa.

"Amekuja kwa ajili ya majaribio na si kwamba tunamsajili kwani dirisha limefungwa, idadi ya wachezaji wa kigeni pia imetimia ingawa ameonekana kuwa ni mchezaji mzuri, kama kocha atamkubali tunaweza kumsajili kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika endapo kanuni pia zitaruhusu vinginevyo ni mpaka msimu ujao wa Ligi Kuu," alisema kiongozi huyo.


Naya kocha Hans Pluijm alisema kuwa "Natakiwa nipewe muda kumwangalia ili kumtolea tathimini, kwasasa nitakuwa muongo kwani ndiyo kwanza anaanza majaribio, muda ukifika nitaweka wazi mtazamo wangu juu ya mchezaji huyu," alisema Pluijm

Takwimu zinaonyesha kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 ameichezea timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 pindi akizichezea timu za Police na Rayon Sports za Rwanda pamoja na DC Vilunga ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Post a Comment

 
Top