BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
YANGA imempa mkataba wa mwaka mmoja Kiungo wao mpya Issoufou Boubacar 'Diego' ambaye amefanyiwa vipimo vya afya leo hii ambapo pia wanatarajia kumsainisha straika Paul Nonga wa Mwadui FC ya Shinyanga anayetarajiwa kutua kesho asubuhi jijini Dar es Salaam kumalizana na Wanajangwani hao.


Nonga amekuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaotoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha Mwadui kilicho chini ya kocha Jamhuri Kihwelu 'Julio' na kama atafanikiwa kumwaga wino Jangwani basi ataungana na kocha wake wa zamani wa Mbeya City, Juma Mwambusi pamoja na kiungo Deus Kaseke.

Habari kutoka Yanga pia zinaeleza kuwa uongozi wa timu hiyo umempa ajira Daktari David Tesha huku ikiachana na Daktari wao Matuzya.


Nonga alikiri kufanya mazungumzo ya awali na Yanga ambao wamepanga kumpa mkataba wa mwaka mmoja "Ni kweli nakuja kesho asubuhi kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho, hii ni kazi yangu na popote pale natakiwa kufanyakazi ili mradi napata fedha ninayoihitaji, tukimalizana nitasaini,"

Post a Comment

 
Top