BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo wameendeleza ushindi kwa kuifunga Mbeya City bao 3-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo kufikisha pointi 33 na kuendelea kung'ang'ania kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo.


Straika wa Yanga, Amissi Tambwe ndiye aliyeanza kutikisa nyavu za Mbeya City ukiwa ni mpira wa krosi uliopigwa na Simon Msuva na kumpata mchezaji wa Yanga aliyeupiga kwa Tambwe ambaye aliumalizia kwa kuudumukiza nyavuni.

Kwa mabao hayo mawili ya Tambwe amefikisha mabao kumi na kumzidi  straika Elius Maguli wa Stand United mwenye mabao tisa.

Yanga walikosa mabao mengi kipindi cha kwanza na umahiri wa kipa Juma Kaseja aliweza kuokoa hatari nyongi ikiwemo ya Thaban Kamusoko aliyepiga shuti kali huku kila mmoja akiamini ni bao.


Safu ya ushambuliaji ya Mbeya City ilionekana kushindwa kufanya mashambulizi na kumfanya muda mwingi kipa wa Yanga, Deogratius Munishi 'Dida' kutokiwa na kazi nguvu ya kuokoa mashambulizi.

Kipindi cha pili Yanga waliongeza mashambulizi huku City ikiwa inacheza pungufu baada ya beki wao Tumbe Swedi kulimwa kadi nyekundu ambapo Tambwe aliongeza bao la pili dakika ya 64 alilofungwa kwa kichwa ukiwa ni mpira wa kona uliopigwa na Haji Mwinyi huku Kamusoko akiongeza bao la tatu dakika ya 66.

Mbali na Tumba kupewa kadi nyekundu Mwamuzi wa mchezo huo Jeonisia Rukyaa alitoa kadi za njano kwa wachezaji wengine wa Mbeya City, Haruna Shamte na Them Felix.

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm alifanya mabadiliko kipindi cha pili ambapo aliwatoa Donald Ngoma, Deus Kaseke na Msuva nafasi zao zilichukuliwa na Paul Nonga, Matheo Anthony na Mniger Issoufou Boubacar.

Post a Comment

 
Top