BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo wameshindwa kutamba mbele ya maafande wa Mgambo JKT baada ya kukubali sare tasa katika mechi ya ligi iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Azam ambayo pia imelazimisha sare ya bao 2-2 na Simba kuendelea kuwa kileleni kwa pointi 26 huku Yanga wakishika nafasi ya pili kwa pointi 24, Mtibwa Sugar ambao pia wametoka sare na Mbeya City ya bao 2-2.

Said Bahanuzi(11) akishangilia bao lake dhidi ya Mbeya City


Mbeya City ndiyo walioikaribisha Mtibwa kwenye uwanja wa Sokoine ambao mabao yao yalifungwa na Haruna Moshi 'Boban' na Issah Nelson wakati mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Said Bahanuzi na Ally Sharif.

Simba itaendelea kushika nafasi ya nne ikiwa na pointi 22 ambapo mechi ijayo wataenda kucheza ugenini dhidi ya Toto African ya jijini Mwanza na baadaye wataenda Shinyanga kucheza na Mwadui FC.

Matokeo mengine katika mechi za ligi, Stand United imekubali kipigo cha bao 2-0 mechi iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga huku Kagera na Ndanda Fc nao wametoka sare ya bao 1-1, mechi iliyochezwa Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.

Post a Comment

 
Top