BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda kwa msaada wa mitandao


Liverpool yaizima Leicester 1-0

REKODI ya vinara wa ligi kuu nchini Uingereza, Leicester City, ya kutopoteza mchezo katika mechi tisa mfululizo  ilivunjwa jana kwa bao la Christian Benteke aliyeingia dakika 38 kuchukua nafasi ya Divock Origi aliyeumia.

Benteke alifunga bao hilo katika kipindi cha pili na kuifanya Liverpool iungane na Manchester City pamoja na Tottenham katika kusherehekea 'Boxing Day' kwa furaha baada ya ushindi.Chelsea bado 'ipo gonjwa'

Meneja mpya wa Chelsea, Guus Hiddink alipata wakati mgumu kazi yake mpya baada ya timu yake kubanwa mbavu na Watford na kuambulia pointi moja tu katika sare ya mabao 2-2.

Shukrani kwa mabao mawili ya Diego Costa ingawa mabao ya Troy Deeney na Odion Ighalo wa Watford yaliinyima ushindi Chelsea.De Bruyne atisha, aing'arisha Man City

Straika wa Manchester City, Kelvin De Bruyne jana alikuwa nyota wa mchezo dhidi ya Sunderland baada ya kutengeneza mabao mawili huku akifunga moja katika ushindi mnono wa mabao 4-1.

Raheem Sterling, Yaya Toure na Winfred Bony ambaye alikosa penati, waliipatia Man City mabao mengine huku Fabio Borin akiipatia Sunderland bao la kufutia machozi.Kane kama kawaida, aipaisha Tottenham

Mshambuliaji Harry Kane alikuwa kwenye kiwango chake baada ya kuipatia timu yake mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata dhidi ya Norwich City. Tom Carrol aliipatia Spurs bao la tatu.


Man United yaangukia pua

Katika mechi ya mapema kabisa, Manchester United ambayo ipo katika msimu mbaya iliambulia kichapo cha mabao 2-0 kwenye uwanja wa Brittania dhidi ya Stoke City. Bojan Krjkic akiweka kwenye nyavu mabao yote mawili.


Arsenal 'majanga'

Kama wangeshinda jana dhidi ya Southampton basi Arsenal ingekaa kileleni mwa ligi, lakini kilichotokea ni majanga. Mabao mawili ya Shane Long pamoja na yale yaliyowekwa  nyavuni na Cuco Martina na Jose Miguel Fonte yalitosha kuisambaratisha Arsenal kwa ushindi mnono wa mabao 4-0.


Post a Comment

 
Top