BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba kwa Msaada Wa Mtandao
CRYSTAL Palace imemsajili Emanuel Adebayor aliyekuwa hana timu baada ya Tottenham  Hotspur kumtema  na mara baada ya usajili huo alisema kuwa anataka avunje rokodi ya Didier Drogba kuwa mwafrika aliye funga mabao mengi zaidi katika ligi kuu ya Uingereza. 


Drogba amefunga mabao  104 na Adebayor yuko nyuma kwa mabao manane tu ili afikie rekodi hiyo.

Pia mshambuliaji huyo  raia wa Togo  aliyewahi kucheza Arsenal, Manchester  City, Tottenham Hotspur na Real Madrid alisema ilikuwa inamuwia vigumu kukaa nje ya uwanja  bila ya  kucheza mechi za kimashindano.  

 Hata hivyo Adebayor alisema  hata kama  watu walikua hawamuoni akicheza  ila alikuwa akiendelea kufanya mazoezi ya mpira katika kipindi hichi  kigumu kwake. Ikumbukwe Adebayor  amecheza dakika 17 tu tokea Januari 2015 .   

Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa aliichagua  Crystal  Palace kwavile kuna marafiki zake pale na anapenda ligi  kuu ya Uingereza ingawa zilikuwepo ofa nyingi.

Post a Comment

 
Top