BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
MLINZI wa kati wa timu ya Azam FC Aggrey Moris Chacha baada ya kuumia katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar Herroes, leo majira ya alasiri ameelekea Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi.


Aggrey ambaye hajaonekana katika kikosi cha Azam tangu ligi kuu isimame kupisha majukumu ya timu za Taifa kwenye michuano ya CECAFA. Aliumia wakati Zanzibar Herroes ikijiandaa kwenda Ethiopia.

Mlinzi huyo hodari ameondoka leo alasiri akiongozana na daktari wa timu ya Azam Dr. Juma Muimbe ambaye ni mmoja wa madaktari wazalendo katika timu ya Azam.

Aggrey anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti na atakuwa huko kwa takribani wiki moja  kimatibabu kabla ya kurejea nchini kuendelea na tiba kutokana na maagizo ya wataalam wake.

Tayari wachezaji kama Michael Balou, Joseph Kimwaga, Frank Domayo, Mcha Khamis na Haji Nuhu walishakwenda nje ya nchi kutibiwa na kurejea katika viwango vyao.

Post a Comment

 
Top