BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
SHUJAA wa Taifa la Tanzania aliyetwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka kwa wanaocheza ndani, Mbwana Samatta, anatarajiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuanzia majira ya saa 8 usiku.

Yaweza kuwa kichekesho lakini huo ndio ukweli kwamba Straika aliyeipatia heshima kubwa sana Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla ataingia muda ambao watanzania wengi watakuwa wamelala tena usingizi mzito na kwamba wachache sana ndio watafanikiwa kushuhudia nyota huyo wa TP Mazembe akiwasili nyumbani na tuzo yake.

Hii ni tofauti kabisa na hali ilivyokuwa nchini Gabon nyumbani kwa Mchezaji Bora wa Mwaka Afrika, Pierre Aubameyang. Rais wa nchi hiyo Ali Bongo aliweka picha katika akaunti yake ya mtandao wa Twitter zikionyesha jinsi shujaa wao huyo alivyopokelewa kifalme tena mchana kweupe.

Uongozi wa chama cha Soka nchini Tanzania, TFF, umeshindwa kufanya mabadiliko ya tiketi ya Samatta ili kumuwezesha kuwasili nchini muda mzuri ambao watanzania wengi wangempokea na kushuhudia tuzo hiyo. Limekuwa ni jambo la ajabu ambalo wadau wengi wa Soka wameshinda kutwa ya leo wakilipigia kelele.BOIPLUS tayari imejipanga kuwepo uwanja ili kuwahabarisha watanzania wengi watakaoshindwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria. Tutakuwa tukiweka matukio yote, kadiri yanavyotokea, kwenye akaunti zetu za Twitter @BoiplusBlogspot na Instagram @boiplus_blogspot. Baada ya kumalizika kwa tukio hilo tutawaletea stori nzima hapa kwenye Blogsite yetu


Post a Comment

 
Top