BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu, Chamazi
VINARA wa ligi kuu ya Vodacom, Azam Fc wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanaiacha Azam kileleni ikiwa na pointi 36 huku Yanga itakayocheza na Ndanda Fc kesho Jumapili ikishika nafasi ya pili na pointi 33.


Azam ilipata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Frank Domayo aliyefunga kwa shuti kali nje ya eneo la hatari baada ya kumpunguza beki mmoja wa African Sports.

Kipindi cha pili, Sports walikuja kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Hamad Mbumba aliyefunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.


Azam ilijitahidi kurejea mchezoni kusaka bao la ushindi ambapo kocha Stewart Hall aliwatoa Domayo na Waziri Salum na kuwaingiza Mudathir Yahya na Farid Mussa lakini hadi dakika ya mwisho matokeo yalikuwa 1-1.


Azam imekuwa na matokeo mabovu hivi karibuni baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi katika hatua ya makundi kabla ya kupata sare hii leo.

Post a Comment

 
Top