BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
HATIMAYE Azam FC imetolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mafunzo jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan.Mabao ya Mafunzo yalifungwa na Rashid Abdallah na Habibu Sadiki huku lile la Azam likiwekwa kimiani na Kipre Tchetche.

Kutokana na matokeo hayo, kikosi cha Azam kitapanda Boti na kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom ambayo imesimama kupisha kombe la Mapinduzi.

Mafunzo yenyewe pia licha ya kushinda mchezo huo, imeshindwa kukuingia hatua ya nusu fainali hivyo kuondolewa mashindanoni na kuziacha Yanga na Mtibwa zinazopambana usiku huu zikisonga hatua ya nusu fainali bila kikwazo.


Huu ni msimamo wa makundi kabla ya mechi za leo

Post a Comment

 
Top