BOIPLUS SPORTS BLOG


RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia (AFC) na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa amewasili nchini leo mchana na kupokelewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.

Sheikh Salman amekuja nchini kwa matembezi ya siku ya mbili na atakuwa na mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Kesho Jumanne, Sheikh Salman Bin Ebrahim Ali Khalifa atamtembelea  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel.


Katika hatua nyingine, TFF limetuma salamu za rambirambi kwa klabu ya Simba SC, kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo miaka ya 1998-2000, Seleman Said ‘Yeltisn’ kilichotokea leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

Katika salamu hizo TFF imesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo, ambaye alingoza klabu ya Simba SC na kupelekea kupewa jina la utani la  Yelstin kutokana na ufanisi wake katika kazi na misimamo akifananishwa na aliyekua Rais wa kwanza Urusi wakati huo Boris Yeltsin.

TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole familia ya Seleman Said ‘Yelstin’ ndugu jamaa, marafiki, uongozi na wanachama wa klabu ya Simba kufuatia kifo hicho, na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.

Mazishi ya marehemu Selaman Said ‘Yelstin’ yanafanyika leo saa 10 kamili jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top