BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda

STRAIKA Mbwana Samatta amefuzu vipimo vya afya na kusaini mkataba wa kuichezea KRC Genk ya nchini Ubelgiji hadi mwaka 2020.

Habari ambazo BOIPLUS imezipata kutoka Genk ni kwamba kapteni huyo wa Taifa Stars alimaliza kila kitu akabaki kumsubiri Rais wa TP Mazembe Moise Katumbi amalize 'shoo' jambo ambalo tayari limeshakamilika. 

"Samatta ameshasaini mkataba wa miaka minne hapa tayari, sasa ni mchezaji wa Genk na atajiunga na timu mara moja." kilisema chanzo chetu.

Picha na video za matukio yote ya vipimo vya afya pamoja na kusaini zitawajia hapa pamoja na kwenye ukurasa wetu wa Instagram (@boiplus_blogspot) baada ya muda kidogo.

Post a Comment

 
Top