BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
STRAIKA wa zamani wa Simba na Gor Mahia, Dan Sserunkuma leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuchezea timu ya Bandari FC ya jijini Mombasa, Kenya.

Bandari inajiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho hivyo inafanya usajili kuimarisha kikosi chake kiwe chenye ushindani mkubwa.


Straika huyo ambaye amewahi kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Kenya (KPL) alishindwa kutamba alipotua Simba na kuamua kuvunja mkataba na kutimkia soka la kulipwa nchini Almania.

Mwishoni mwa mwaka jana, Dan ambaye ni raia wa Uganda aliamua kurudi nchini Kenya ambako familia inaishi huko na kuanza kusaka timu nyingine baada ya kile kilichoelezwa kuwa maisha ya soka ya Almania kumshinda.Dan amekiri kusaini mkataba na Bandari na kwamba yupo tayari kuichezea timu hiyo ingawa hakutaka kuzungumzia zaidi sababu za yeye kuondoka huko ila amesema aliagana nao vizuri tu.

Post a Comment

 
Top