BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KAMA nyie mnadhani Ligi Kuu Bara ndiyo inakwenda ukingoni basi wenzenu Coastal Union ndio kwanza kwao ligi ni mbichi kabisa.


Kauli hiyo imetokea baada ya kufanikiwa kuwafunga mabingwa watetezi wa VPL, Yanga mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Adam Miraji ndiye alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za wapinzani wao ikiwa ni dakika ya 27 tangu mchezo uanze na amesema kuwa hawatakubali tena kupoteza mechi kwani wanapigana ili wawe na uhakika wa kubaki kwenye ligi.

"Tumeanza ligi rasmi leo, tumewafunga mabao mawili dakika za mwanzo za kila kipindi, mabao ambayo yaliwachanganya na kushindwa kurudisha. Mwenendo wetu haukuwa mzuri ila sasa tumefungua rasmi kitabu cha mabao.

"Wanasema kila jambo lina wakati wake ndivyo ilivyo hata kwetu na kwangu pia ambaye nawaza mbele zaidi na nitafika ninapopahitaji, Yanga ni timu ya kawaida kwa upande wa uchezaji ila wana jina kubwa," alisema Miraji

Bao la pili la Coastal Union lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 62 na Juma Mahadhi bao ambalo liliwavuruga zaidi Yanga.

Post a Comment

 
Top