BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KIUNGO wa Ndanda FC, William Lucian 'Gallas' amekichambua kikosi cha Mgambo JKT na kutamka kwamba ameona mchezaji mmoja tu Fully Maganga kuwa ndiye anayetegemewa na wamemfuatilia nyendo zake.Ndanda na Mgambo watakutana keshokutwa Jumapili kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga na leo mchana wameondoka mkoani Pwani walikokuwa wamepiga kambi na kuwafuata wapinzani wao hao.

Gallas amesema kuwa wanawafahamu wapinzani wao kwani wamewahi kukutana kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza na kulazimisha sare ya bao 1-1, mechi iliyochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaoni mkoani Mtwara.

Beki huyo ambaye aliwahi kucheza kwa mafanikio akiwa Simba, alisema kuwa kikubwa wanachotakiwa kukifanya kwasasa ni kuhakikisha wanapigania pointi tatu kwa kila mechi ili timu yao ibaki kwenye ligi.

"Mechi za mwishoni mwishoni zinakuwa ngumu sana kwasababu kila timu inapambana kubaki kwenye ligi ama kutwaa ubingwa, timu yetu ni nzuri na wapinzani wetu wajao ni wazuri ila wao wanamtegemea mchezaji mmoja tu, Maganga ambaye tunajuwa mbinu zake," alisema Gallas

Post a Comment

 
Top