BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
VUTA nikuvute ya muda mrefu kati ya mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi na Mbwana Samatta imemalizika jana Ijumaa baada ya mmiliki huyo kukubali mshambuliaji wake kuondoka kwenda kumalizana na KRC Genk ya Ubelgiji.Samatta anatarajia kuondoka usiku wa leo kuelekea Ubelgiji ambako atasaini mkataba wa miaka minne na nusu ukiachana na ule wa awali aliokuwa amesaini kabla ya Genk kumalizana na Katumbi jambo ambalo lilizua mtafaruku ambao uliingiliwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo.

Katika msafara huo wa kwenda Ubelgiji, Samatta ataambatana pia na bosi wake Katumbi ambaye atashuhudia usainishwaji wa mkataba huo.

"Baada ya majadiliano ya muda mrefu hatimaye Katumbi amekubali kumwachia Samatta hivyo ataondoka leo usiku kwenda Ubelgiji kumalizana nao kabisa. Akimaliza atarejea nchini kwa ajili ya maandalizi yake ya kwenda kuitumikia klabu hiyo mwezi ujao," alisema mtu wa karibu wa Samatta.

Jana Meneja wake, Jamal Kasongo alisema kuwa walikuwa na kikao na serikali pamoja na mwanasheria wao kikao ambacho kinaonyesha kuzaa matunda.

Post a Comment

 
Top