BOIPLUS SPORTS BLOG

Mbwana Samatta ametwaa tuzo ya mchezaji Bora wa mwaka wa Afrika kwa ligi za ndani kwa kupata kura 127 huku wapinzani wake, Robert Kidiaba akipata kura 88 na Baghdad Bounedjah akiambulia kura 63.

Baada ya tukio hilo lilifuata zoezi la kusherehekwa kwa kupiga picha nyingi tu, lakini alipomaliza na kwenda kulala ndipo ilipopatikana picha Bora kabisa ya siku nzima.

Samatta anaonekana akiwa kitandani amesinzia huku akiwa amejifunika bendera ya Taifa la Tanzania na pembeni kukiwa na tuzo yake hiyo ambayo yeye ni mchezaji wa kwanza si tu kwa Tanzania, bali ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati kuitwa.

Tazama picha hii hapa chini.

Post a Comment

 
Top