BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MSHAMBULIAJI wa Simba, Raphael Kiongera atakaa nje kwa wiki mbili akiwa anauguza majeraha yake huku beki Mohamed Hussein 'Tshabalala' yeye akitarajiwa kurudi uwanjani wiki ijayo.


Kiongera atalazimika kukosa mechi tatu kuanzia kesho Jumamosi dhidi ya African Sports na mechi nyingine ya Kagera Sugar pamoja na Stand United zitakazopigwa mkoani Shinyanga.

Kiongera amesema kuwa baada ya vipimo alivyofanyiwa Jumanne ya wiki hii atalazimika kukaa nje kwa ajili ya kujiuguza ingawa hali yake kwasasa inaendelea vizuri ukilinganisha na hapo awali.

"Nimeambiwa nipumzike wiki mbili, hivyo nitakuwepo tu, naamini nitakaa poa na kurudi uwanjani," alisema mshambuliaji huyo ambaye kwasasa anakabiliwa na ukame wa mabao kwani hajafunga bao hata moja tangu arudi Simba akitokea KCB alikokuwa akicheza kwa mkopo.


Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema kuwa wachezaji hao wawili wanaendelea vizuri na anatarajia kuanzia wiki ijayo watarudi uwanjani 

"Wengine wote akiwemo Ibrahim Ajibu wako fiti kabisa kasoro Tshabalala na Kiongera ila wanaendelea vyema,".

Post a Comment

 
Top