BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Marco Ngavenga, Mbeya
KOCHA Mkuu wa timu ya Kimondo ya wilayani Mbozi, Anton Mwamlima amejiuzulu kuinoa timu hiyo kwa kile alichodai kutingwa na matatizo ya kifamilia.


Mwamlima ameiambia BOIPLUS kuwa amechukuwa uamuzi huo ili kushughulikia matatizo yake na si vinginevyo kwani muda mwingi alikuwa akiutumia kwenye timu hiyo.

"Nimeona nikae pembeni ili kutosababisha mambo mengine  kwenye timu, kwani nimeona siwezi kumudu majukumu mawili kwa pamoja, kwa màana ya kufundisha timu huku nikishughulikia matatizo ya familia yangu," alisema Mwamlima.

Alipoulizwa kuwa pengine uamuzi wake umetokana na timu hiyo kusuasua kwenye ligi Daraja la Kwanza alisema "Sio kweli kabisa, ujue tangu niachiwe mikoba na Maka Mwaluwisi, nimefanya usajili wa maana na nimecheza mechi nne, nimeshinda mbili, sare moja na nimefungwa mechi moja na timu ina pointi 11 ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo''.

Mkurugenzi wa klabu hiyo, Erick Ambakisye alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya hilo hakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa kile alichodai kuwa alikuwa kwenye kikao.

Post a Comment

 
Top