BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
MSHINDI wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wanaocheza ligi ya ndani, Mbwana Samatta ametua salama nchini saa 8.30 usiku huu akitokea Abuja, Nigeria alikotwaa tuzo hiyo.Licha ya kutua usiku wa manane bado mashabiki kibao wa soka walijazana kumpokea huku wakiimba jina lake na kucheza kwa furaha katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA)

Waandaaji wa shughuli hiyo ya mapokezi walipanga Samatta azungumze na waandishi wa habari mara baada ya kutua lakini mashabiki waliojazana walimvamia na kuanza kumshangilia na kusababisha taratibu zote zilizoandaliwa hapo awali zivurugike. 

Kutokana na hilo ililazimika Samatta aingizwe kwenye gari maalumu na kupelekwa moja kwa moja katika Hotel ya Serena ambako alizungumza na waandishi wa Habari.


Samatta amewashukuru watanzania kwa moyo wa upendo waliomuonyesha huku akiwasihi wachezaji wa hapa nchini waongeze bidii ili waweze kufanikiwa.

"Nimefarijika sana na nawashukuru kwa ushirikiano mliyonipa, hii ni tuzo ya Watanzania wote. Wachezaji nawashauri waongeze juhudi zaidi ili kufikia mafanikio,'' alisema Samatta

Post a Comment

 
Top