BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Abra David kwa Msaada wa mitandao
JARIDA la Deloitte  limeufahamisha Ulimwengu kuwa Klabu inayotokea nchini Hispania,  Real Madrid ndio klabu inayojiingizia mapato mengi kuliko klabu yoyote katika mchezo wa mpira wa miguu duniani.Madrid imeingiza mapato ya euro 577 milioni, ambayo asilimia 22 yametokana na viingilio vya mechi, asilimia ya 43 matangazo ya biashara na aslimia 35 inatokana na vyanzo vya maonesho ya mechi katika vituo mbalimbali vya televisheni.

Katika orodha hiyo ya klabu bora 20 vinavyoingiza mapato zaidi duniani imezitaja klabu 9 zikitokea ligi ya Uingereza ambazo ni Manchester City, Manchester United, Liverpool, Newcastle, West Ham United, Arsenal, Everton, Tottenham na Chelsea.

Ligi ya Uingereza ndio ambayo imetoa klabu nyingi katika orodha hiyo ya klabu tajiri huku ligi ya Italia maarufu kama seria A ikiwa imetoa klabu nne ambazo ni Ac Milan, Juventus, Inter Milan na As Roma. Bundes liga imetoa klabu tatu zikiwa ni Schalke 04, Borussia Dortmund na Bayern Munich.

Ligi ya Hispania almaarufu La Liga imetoa klabu tatu ambazo ni matajiri hao wa kwanza Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid. Ligi ya Ufaransa inayofahamika kama Ligue One imetoa timu moja Paris St Germain timu ya tajiri inayomilikiwa na Nasser Al-Khelaifi

Post a Comment

 
Top