BOIPLUS SPORTS BLOG

HALI bado ni tete kwa kocha wa Real Madrid, Rafael Benitez baada ya leo kikosi chake kuambulia sare ya mabao 2-2 ilipoitembelea Valencia.

Karim Benzema aliitanguliza mbele Madrid kwa bao safi la dakika ya 16 akimalizia pasi ya nyuma ya Cristiano Ronaldo ambaye alipokea pasi ya kisigino toka kwa Gareth Bale.


Dakika ya 45 Parejo aliisawazishia Valencia kwa mkwaju wa penati iliyotokana na Pepe kufanya madhambi kwenye eneo la penati. 

Kipindi cha pili Madrid walipata pigo baada ya kiungo wake Matheo Kovacic kuzawadiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Valencia


Dakika ya 82, Bale aliipatia Madrid bao la pili kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliochongwa na Toni Kroos lakini dakika moja baadaye, yani dakika ya 83, Francisco Alcacer aliisawazishia Valencia kwa bao maridadi akiitumia vema krosi ya Rodrigo.

Post a Comment

 
Top