BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu
TIMU ya Mtibwa Sugar imesema ipo tayari kuivaa African Sports katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku wakijihakikishia kuondoka na pointi tatu muhimu.Mtibwa wanaingia uwanjani wakiwa na hasira ya kupoteza mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0 wakati wapinzani wao African Sports walitoka sare ya bao 1-1 na Azama FC.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Meck Mexime alisema wamejipanga vizuri kuzisaka alama tatu katika mchezo huo utakaopigwa Jumamosi.

"Tunakwenda Tanga kupapamba ili kupata pointi tatu, hatuangalii matokeo ya mechi iliyopita, tunajiandaa kikamilifu na tutaondokea Morogoro kuwafuata wapinzani wetu," alisema Mexime

Mtibwa Sugar imejikusanyia pointi 27 mpaka sasa wakishika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakitanguliwa na Yanga wenye pointi 36 sawa na Azam Fc huku Simba wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 30.

Post a Comment

 
Top