BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba Kwa Msaada Wa Mitandao
MBRAZILI Ramires  amekamilisha  uhamisho wa kujiunga na Jiangsu Suning  inayoshiriki ligi kuu China akitokea Chelsea. Inasemekana Ramires ameuzwa euro  25 milioni  ingawa haijatajwa wazi.


Ramires  ameitumikia Chelsea kwa miaka mitano na nusu na kuifungia mabao 36 katika mechi 254 alizoichezea miamba hiyo yenye uwanja wa Stamford Bridge.

 Ramires amekuwa na  wakati mgumu chini ya Gus Hiddink  kwa kutopata nafasi katika kikosi cha kwanza  na hilo ndilo inasemekana limemshawishi Ramires atimkie nchini Chini.

Jiangsung inafundishwa na aliyewahi kuwa mchezaji wa Chelsea  Dan Petrescu.

Post a Comment

 
Top