BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
STRAIKA wa Gor Mahia FC,  Michael Olunga amefanya mazungumzo ya awali na klabu ya Djurgardens IF  ya Sweden lakini amesema kuwa bado hajamalizana nao hivyo ataendelea kuitumia timu yake ambao ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu Kenya (KPL).


Olunga ambaye alitwaa tuzo ya Mfungaji Bora katika tuzo za Foya msimu uliyopita baada ya kuifungia timu yake ya  Kogalo mabao 19,
amekiri kufanywa kwa mazungumzo hayo na kama watafika makubaliano basi anaweza kwenda kukipiga Ulaya.

Mwaka jana straika huyo alikuwa akiwaniwa na vigogo wa soka nchini Simba na Yanga lakini walishindwa kumng'oa kutokana na dau kubwa lililokuwa likitajwa huku akitaka mkataba wake uwekwe kipengele cha kuendelea na masomo yake ya Chuo Kikuu.

"Ni kweli nimefanya mazungumzo na timu hiyo lakini sijasaini nao mkataba mimi kwa sasa bado ni mhezaji wa Gor Mahia," alisema Olunga

Olunga alishiriki pia tuzo za Foya ya Mchezaji Bora zilizofanyika wiki iliyopita katika Jumba la Mikutano la KICC,  jijini Nairobi lakini hakubahatika kutwaa na mabadala yake ilikwenda kwa mrusha mkuki bingwa wa dunia, Julius Yego.

Wengine waliobwagwa na mrusha mikuki huyo ni Jesse Were, Meddie Kagere, Karim Nizigiyimana, Bernard Mang'oli na Ebrimal Sanneh

Post a Comment

 
Top