BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, amekipongeza kikosi chake kwa kuibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Ndanda FC uliochezwa  katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. 


Yanga walikuwa wenyeji wa mchezo huo na kufanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 bao ambalo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Kelvin Yondani na kuifanya timu hiyo kupanda kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 36 sawa na Azam ingawa Yanga ina mabao mengi ya kufunga.

Akizungumza baada ya pambano hilo, Pluijm alisema ushindi ni ushindi hata kama wamefanikiwa kupata bao moja bado wamewambulia pointi tatu. 

Alisema ataendelea kukisuka kikosi hicho ili kiweze kuendelea kuibuka na ushindi katika michezo iliyobaki na kuweza kutetea ubingwa wa Ligi Kuu wanaoushikilia. 

Wakati Pluijm akitamba na kikosi chake, kocha wa Ndanda, Hamimu Mawazo yeye ameilamu safu yake ya ushambuliaji kwa kushindwa kuzitumia vizuri nafasi walizozipata.

 "Wachezaji wangu wamecheza vizuri na wametengeneza nafasi nyingi lakini wameshindwa kuzitumia nitajitahidi kuyarekebisha makosa yaliyojitokeza naamini tutafanya vizuri katika michezo ijayo," alisema Mawazo

Post a Comment

 
Top