BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm amesema kuwa kamwe hawawezi kubweteka kwa kuona watani wao Simba wamemtimua kocha wao Dylan Kerr na kwamba anaendelea kupambana ili atetee ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.Simba imemtimua Kerr pamoja na kocha wa makipa Idd Salim raia wa Kenya kwa sababu tofauti ikiwemo timu kucheza chini ya kiwango kwenye mechi za ligi pamoja na Kombe la Mapinduzi ambapo walishindwa kutetea ubingwa wao.

Pluijm ambaye pia timu yake ilitolewa kwenye michuano hiyo alisema kuwa mabadiliko yaliyofanywa na Simba yanamfanya awe makini katika mechi zake zijazo za ligi kuu.

"Ni mara nyingi Simba wamekuwa wakiwatimua makocha wao, hayo ni maamuzi yao kama timu na siwezi kuingilia na ni jambo ambalo haliwezi kutuathiri ila tunajipanga zaidi kutetea ubingwa kwa kushinda mechi zilizobaki.

"Ligi ni ngumu na kwenye mbio za ubingwa hutakiwi kubweteka na misukosuko ya Simba. Hatutakiwi kuiangalia Simba pekee sasa tunaangalia mechi zote zilizobaki kuhakikisha tunashinda, kikosi changu kipo vizuri tu,'' alisema Pluijm

Yanga wanajiandaa na mechi dhidi ya Ndanda FC itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top