BOIPLUS SPORTS BLOG

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa timu ya Taifa Stars na TP Mazembe, Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza barani Afrika.


Sherehe za tuzo hizo zilifanyika jana Alhamisi usiku katika Mji wa Abuja nchini Nigeria na anatarajia kurejea nchini saa 8 usiku, ambapo amemtaka Waziri Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwana imesema kuwa tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya soka Kimataifa.Aidha, Rais Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.

Post a Comment

 
Top