BOIPLUS SPORTS BLOG

MIAMBA ya soka ya Hispania Real  Madrid walio chini ya kocha  wao mpya Zinedine  Zidane na Atletico Madrid wanaofundishwa na Diego Simeone wamepatwa na majanga kama waliyowahi kupata  wenzao  Barcelona baada ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA kuzifungia klabu hizo kutosajili kwa vipindi viwili vijavyo vya usajili.


Adhabu hiyo iliyoambatana na faini ya Paundi 662,000 kwa Madrid na Paundi 249,000 kwa Atletico imetokana na klabu hizo kuvunja kanuni za usajili kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 18. 

Wakati mwenzao Barcelona akiwa anamaliza kifungo, wao wanaanza kutumikia adhabu hiyo ambapo hadi sasa kuna mjadala endapo timu hizi zitaruhusiwa kusajili katika dirisha la Januari au vinginevyo.
  
Kifungo  hiki kinaweza kuiathiri zaidi Real Madrid ya Zidane kutokana na nia yake ya  kubadili kikosi kwa kuleta sura  mpya kama David De Gea, Paul Pogba na wengine.

Post a Comment

 
Top