BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta, ameandika historia kwa kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa Afrika kwa wanaocheza ligi za ndani. 

Samatta anakuwa mtanzania wa kwanza kutwaa tuzo hiyo huku akiwa ametoka kuandika historia nyingine miezi michache iliyopita pale yeye na Thomas Ulimwengu walipokuwa watanzania wa kwanza kutwaa taji la ligi ya ya Mabingwa Afrika.

Samatta amewashinda wapinzani wake Robert Kidiaba na Baghdad.

Kwa upande mwingine, tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla imekwenda kwa Pierre Aubameyang ambaye amewashinda Andre Ayew na Yaya Toure.

Post a Comment

 
Top