BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
WASHAMBULIAJI wawili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Farouk Miya wa Uganda na Michael Olunga raia wa Kenya ambao mwaka jana walikuwa wakitajwa kuwaniwa na Simba ya jijini Dar es Salaama sasa mambo yao safi kwani wanakwenda kukipiga Ulaya huku mmoja pia kutoka Kenya akitimkia Zambia.

Mshambuliaji wa Vipers ya Uganda, Farouk Miya

Wachezaji hao wote wanazichezea pia timu za Taifa za mataifa yao wamefanikiwa kwenda kukipiga Ulaya na huku Miya akitarajiwa kuondoka muda wowote kwenda Standard Liege ya Ubelgiji, Olunga yeye tayari ameshawasili nchini Sweeden katika klabu ya IF Djurgardens. Jesse Were ambaye ni Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Kenya (KPL) yeye amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Zesco.

Standard Liege ilionyesha nia ya kumsajili mtanzania Mbwana Samatta lakini 'deal' hiyo imeishia njiani huku Wabelgiji hao wakiamua kumchukua Miya kama mbadala wake.

Mbali na wachezaji hao kwenda Ulaya, Gor Mahia ambayo ndiyo mmiliki wa Olunga na Jesse imeanza mchakato wa kumsajili Jacques Tuyisenge raia wa Rwanda na tayari usajili wake umekamili kwa asilimia kubwa.

Wiki iliyopita Olunga alikiri kufanya mazungumzo na timu hiyo na kwamba yupo tayari kwenda huko endapo tu mazungumzo yao ya mwisho yangekamilika ambapo wiki hii imeelezwa kuwa mambo yamekuwa mazuri kwake.

Michael Olunga akiwa nchini Sweeden na timu yake mpya

Kuondoka kwa wachezaji watatu ndani ya Mabingwa wa KPL, Gor  Mahia kutawafanya waanze kutafuta wachezaji watakaoweza kuisadia timu hiyo katika kutetea ubingwa kwenye msimu ujao wa ligi kwani imeondokewa na wachezaji watatu muhimu na tegemezi katika kupachika mabao Jesse na Olunga.

Kocha wa Zesco, George Lwandamina, ambaye kwa sasa anafundisha timu ya Taifa ya Zambia kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) amekiri kufanyika usajili wa Jesse na kwamba kikosi chake msimu ujao kitakuwa imara zaidi.

Post a Comment

 
Top