BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
NYOTA iking'ara, hata mkaa unageuka almasi. Wakati dili ya Mbwana Samatta kwenda KRC Genk ikiwa bado haijatoa majibu yanayoeleweka, nyota ya straika huyo ambaye ni Mchezaji Bora wa Afrika (ligi ya ndani) imeendelea kung'ara baada ya vigogo wa Ligi kuu ya Ufaransa, Olympic Marseille nao kujitosa kumuwania.

Seydou Doumbia....ndiye kashikilia deal ya Samatta

Akiwa nchini DR Congo kwenye klabu yake ya TP Mazembe ambako ameenda kwa lengo kuu la kumshawishi Bosi wake Moise Katumbi akubali kumuuza Genk, Samatta amepokea simu ya Rais wa Marseille inayomtaka kukaa mkao wa kula kwa maana muda wowote anaweza kuitwa kwenda kuvaa jezi .

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka jijini Lubumbashi ni kwamba Samatta amezungumza na bosi wa vigogo hao kwa njia ya mtandao wa Skype na kwamba ameambiwa kuwa wanahitaji straika wa aina yake ila chaguo lao la kwanza ni Muivory Coast anayekipiga CSKA Moscou ya Urusi, Seydou Doumbia ambaye wapo kwenye mazungumzo naye.

Kama Doumbia atagomea dau la Marseille, wafaransa hao watalazimika kumtumia tiketi haraka Samatta ili akamalizane nao kabla dirisha la usajili halijafungwa rasmi.


Hata hivyo mtandao huu unajua kuwa mpango wa Samatta kwenda Genk uko kwenye hatua za mwisho na kwamba muda wowote Mfungaji Bora huyo wa ligi ya Mabingwa Afrika atakwea pipa kwenda Ubelgiji

Post a Comment

 
Top