BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
SIMBA ina pointi nne mpaka sasa baada ya kucheza mechi zake mbili na kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali lakini wamejihakikishia kutetea ubingwa huo wa Kombe la Mapinduzi.

Tayari Azam na Mafunzo wameondolewa kwenye michuano hiyo katika Kundi B baada ya mechi yao ya leo ambapo Azam wamefungwa bao 2-1, mechi iliyochezwa uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.


Beki wa Simba, Emery Nimubona ameiambia BOIPLUS kuwa wana nafasi kubwa ya kutetea ubingwa huo kama waamuzi watachezesha kwa kufuata sheria za soka.

''Mashindano ni magumu ila tumejipanga kutetea ubingwa na kuwapa zawadi hii mashabiki wetu kikubwa tunaomba ushirikiano wao kufanikisha hili, kikosi chetu ni bora zaidi,'' alisema Nimubona.

Nimubona alisema kuwa mashindano hayo pia yanawasaidia kuwajenga na watakaporudi kwenye mechi za Ligi Kuu basi watakuwa kwenye kiwango kizuri zaidi.

''Unajuwa kwa mechi kama ya jana ilikuwa ngumu, URA ni wazuri japokuwa tuliwafunga hivyo kucheza na timu ngumu kunatujenga na tukirudi kwenye ligi tutakuwa imara zaidi,'' alisema

Post a Comment

 
Top