BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
MSHAMBULIAJI na nahodha wa  Taifa Stars, Mbwana Samatta, jana alikamilisha uhamisho wake wa kutua KRC Genk ya Ubelgiji akitokea kwa mabingwa wa Afrika, TP Mazembe ya DR Congo.


Wakati wa utambulisho wake kwa wanahabari Samatta alikabidhiwa jezi namba 77, namba ambayo hajawahi kuonekana akiitumia kuivaa katika tinu zote alizozichezea.

BOIPLUS ilimtafuta Samatta ili kujua kwanini aliamua kuchagua jezi hiyo ambapo alisema kuwa jezi anayoiwaza na ambayo anaamini atakuja kuivaa baada ya muda mfupi barani Ulaya ni yenye namba saba (7) mgongoni.

"Mimi jezi ninayoipenda kuliko zote ni namba saba, ila kwavile hapa Genk tayari jezi hiyo ina mtu basi nikaona nichukue namba 77. Ila ipo siku nitavaa jezi namba saba huku huku Ulaya, acha nifanye kazi." alisema Samatta ambaye ameifungia Mazembe mabao 60 katika mechi 103 alizocheza.

Kwa lugha nyingine ni kwamba Samatta anaamini katika zile tarakimu mbili za namba ya jezi yake kuna moja itadondoka akiwa kwenye harakati zake za soka barani Ulaya hivyo kubaki na moja tu ambayo ndio ndoto yake.

Post a Comment

 
Top