BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba Kwa Msaada Wa Mitandao
MANCHESTER CITY NA WASITISHA MAZUNGUMZO NA MCHEZAJI WAO 
MANCHESTER City wameamua  kusitisha mazungumzo ya kumpa mkataba  mrefu  na mnono kinda raia wa Nigeria, Kelechi Ihenacho  baada ya kutokea sintofahamu nani mmiliki halali  wa kinda huyo wa kutumainiwa anayefanya  vizuri katika jiji la Manchester.


Sintofahamu hiyo imetokea baada ya kutokea makundi mawili yanayo toa madai kila moja ndio mmiliki halali wa Ihenacho (19).  Makundi hayo ni United sSates Based First Eleven Management wanaodai walikuwa  wanammiliki tokea akiwa shule. 

Wawakilishi wengine ni Bright Future wanaosema waliingia nae mskubsliano  alipofikisha miaka 18  kitendo hicho kimeifanya Man  city  iombe   msaada kwa FA na kusitisha majadiliano na kinda huyo aliyeifungia city mabao matano msimu huu.


MANCHESTER UNITED  WAWAFANYIA UNYAMA NEWCASTLE KATIKA USAJILI
LICHA ya kutokumtumia Victor Veldes (34)  katika kikosi cha kwanza  na kumfanya kipa huyo kuonekana si lolote mbele ya David De Gea na Romero, Manchester United wamegoma kumuachia kwenda zake Newcastle kwa mkopo licha ya timu hiyo kuonesha kumhitaji  mhispaniola huyo kwa udi na uvumba kutokana na kuumia kwa kipa wao Krul.


Licha ya kwamba  Veldes anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu lakini Lous Van Gaal kasema hataki kuona kipa huyo  anaenda Newcastle


SOUTHAMPTON YAWAAMBIA HAYA MAN  UTD JUU YA MANE 
BAADA ya kocha wa Southamptom  Koeman kumnunua Charlie Austin tetesi  zikaibuka kwamba Sadio Mane na  Graziano Pelle wanaweza wakaondoka katika klabu hiyo. 


Ghafla kocha huyo akaibuka na kusema hauzi mchezaji yeyote katika dirisha hili la  Januari na wanaodhani kumleta Austin kutoka QPR kunamaanisha atauza wengine wasahau.  Kauli hiyo inawafanya Man United wamsahau Mane ambaye Van Gaal kamtafuta kwa muda mrefu.


MADRID  WAIVAMIA PSG NA KUTAKA KUMNG'OA CAVANI
BAADA ya Real Madrid kula nyundo mbili za kutosajili kwa kosa la kukiuka mikataba ya wachezaji wanaochipukia, wanataka kuji imarisha kupitia dirisha hili la januari kabla adhabu yao haijaanza tekelezwa ktk dirisha lijalo.


 Kwa kutambua ugumu huo, Madrid wamegonga hodi katika jiji la Paris katika klabu ya PSG na kutaka kumng'oa Edson Cavani. Real wanajua Cavani hana Maisha ya  raha kutokana na kutochezeshwa kama mshambuliaji wa mwisho na hiyo ndio faida kubwa  kwa  Madrid  kumnasa mshambuliaji huyo.

Post a Comment

 
Top