BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe leo ameanza mazoezi baada ya kuwa nje akisumbuliwa na maumivu ya sikio lakini amesema hana uhakika wa kucheza mechi yao ijayo dhidi ya Coastal Union.Mechi hiyo itachezwa wikiendi hii katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga na baada ya hapo watasubiri mechi mbili zitakazochezwa jijini Mbeya dhidi ya Prisons na Mbeya City.

Tambwe ameiambia BOIPLUS kuwa "Nimeanza mazoezi lakini bado nasikia maumivu hivyo sina uhakika kama nitacheza mechi ijayo. Nitaangalia kadri siku zinavyokwenda na maumivu yanakuwaje,".

Mpaka sasa Tambwe ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao 13 na kuisaidia timu yake kukaa kileleni ikiwa na pointi 39.


Kwa upande wa majeruhi wengine akiwemo beki Nadir Haroub 'Canavaro' aliyekuwa anasumbuliwa na mkono, Dr Nassoro Matuzya amesema kuwa hali yake inaendelea vyema pamoja na Juma Abdul aliyekuwa akisumbuliwa na malaria naye ameanza mazoezi.

Post a Comment

 
Top