BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally


RAIS Mstaafu, Jakaya Kikwete amempongeza straika Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika kwa mchezaji anayecheza ligi ya ndani katika sherehe zilizofanyika wiki iliyopita jijini Abuja, Nigeria.


Kikwete alisema kuwa Tanzania ilikuwa na kiu ya kupata mwanga kwenye soka hivyo Samatta ameonyesha mwanga huo na kuongeza kuwa hata kiu ya kutwaa makombe mbalimbali kwenye soka ipo siku itakatwa.


''Tulikosa furaha, tulikuwa na ukame wa miaka mingi naamini hata kombe ipo siku tutatwaa, nampongeza sana Samatta amefanikiwa  na amepiga hatua kubwa ila namtaka alenge shahaba zake mbele zaidi hasa kucheza Ulaya ifikie kipindi klabu kutoka Ulaya zije kutafuta vipaji hapa kwetu, naiomba serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kusimamia kuhakikisha wanamsaidia mpaka anafanikiwa," alisema Kikwete.Kwa upande wa Samatta ambaye pia alimkabidhi Rais Kikwete jezi namba tisa aliyokuwa akiitumia Mazembe, aliishukuru serikali na kuweka wazi kwamba maneno aliyowahi kuambiwa na Rais Kikwete yalimfariji na kumjenga kwani yamechangia kwa kiasi kikubwa kupata mafanikio hayo.
Post a Comment

 
Top