BOIPLUS SPORTS BLOG


SHEREHE za utoaji wa tuzo za wachezaji bora wa Afrika zitafanyika usiku wa leo jijini Abuja, Nigeria ambapo karibu mastaa wote walioingia tatu bora wameshawasili tayari. Ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia tatu bora na mafanikio yao.

Mchezaji Bora Africa


Jina: Yaya Toure
Kuzaliwa: Mei 13, 1983
Nchi: Ivory Coast
Klabu: Manchester City


Yaya Toure aliiongoza Ivory Coast kubeba tena kombe la mataifa ya Afrika (AFCON)  tangu walipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 1992. Kabla ya hapo Toure alibeba tuzo hiyo mara nne mfululizo.


Jina: Pierre-Emerick Aubameyang
Kuzaliwa: Juni 18, 1989
Nchi: Gabon
Klabu: Borussia Dortmund


Aubameyang alifanikiwa kuifungia timu yake ya Taifa mabao matano huku pia akiifungia Dortmund mabao mengi.


Jina: Andrew Ayew
Kuzaliwa: Disemba 17, 1989
Nchi: Ghana
Klabu: Swansea City


Ayew aliisaidia Ghana kutinga fainali ya AFCON huku yeye akimaliza akiwa mfungaji bora wa michuano hiyo. Pia amekuwa na mwanzo mzuri kwenye ligi kuu ya England akiwa na klabu yake ya Swansea.


Mchezaji Bora wa Afrika (anayecheza ndani)


Jina: Robert Kidiaba
Nchi: DR Congo
Klabu: TP Mazembe
Umri: 39
Nafasi: Golikipa


Kidiaba ameshinda kombe la mabingwa Afrika akiwa ma Mazembe na kutunukiwa tuzo ya kipa bora wa michuano hiyo


Jina: Baghdad Bounedjah
Nchi: Algeria
Klabu: Etoile du Sahel
Umri: 24
Nafasi: Mshambuliaji


Baghdadaliisaidia Etoil du Sahel kubeba kombe la Shirikisho CAF huku yeye akifunga mabao 6 na kuibuka mfungaji bora.


Jina: Mbwana Aly Samatta
Nchi: Tanzania
Klabu: TP Mazembe
Umri: 23
Nafasi: Mshambuliaji


Samatta ni mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika huku mabao yake hayo yakiwa yameisaidia Mazembe kuibuka mabingwa wa michuano hiyo.

Je, ni nani wataibuka na tuzo hizo leo?.

BOIPLUS inamtakia kila la heri Mbwana Samatta aweze kushinda tuzo hiyo ambayo itailetea heshima kubwa nchi yake Tanzania.

Post a Comment

 
Top