BOIPLUS SPORTS BLOG

BAADA ya kuondolewa katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi huko Zanzibar, mabingwa wa kutandaza kabumbu Tanzania Bara Yanga ya jijini Dar es Salaam, wameamua kuhamishia hasira zao kwenye maandalizi ya Ligi kuu ya Vodacom.


Yanga inajipanga kutetea Ubingwa wake unaonyemelewa kwa karibu na Azam FC huku Mtibwa Sugar waliofungwa na URA kwenye mechi ya fainali ya kombe la Mapinduzi na Simba iliyomtimua kocha wao Dylan Kerr, si za kubeza na zinaweza kuwa tishio katika kampeni hizo.


Kocha mkuu wa timu hiyo Mholanzi Hans Van Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi, wameonekana kuwa makini sana kurekebisha makosa waliyoyafanya Zanzibar huku wakijaribu kuwapa mbinu mpya wachezaji wao.


Wachezaji nao wameonekana wakipambana kuonyesha uwezo wao na kila aina ya ufundi ili kumshawishi kocha kuwaingiza katika kikosi cha kwanza chenye upinzani wa hali ya juu.


Je, Thaban Kamusoko 'Rasta' ataendelea kutisha kwa kutengeneza na kufunga mabao?


Issoufou Boubacar na Vincent Bossou walipata nafasi hivi karibuni na kila mmoja akaonyesha uwezo mzuri, je watafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza?Upinzani katika kikosi cha kwanza unawafanya nyota hawa wa Yanga wageuze mazoezi kuwa kama mechi, hakuna anayekubali kushindwa kwavile wanafahamu bila hivyo wataozea benchi.


Post a Comment

 
Top