BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba kwa msaada wa mitandao
VIDIC  BYE BYE INTER
Nemanja Vidic (34) mzaliwa wa Serbia  ameamua kuingia makubaliano na klabu yake ya Inter Milan ili kuvunja mkataba wake kwa manufaa ya pande zote mbili.


Pamoja na kuichezea Inter mwaka mmoja na nusu, Vidic hakuwa na  maisha mazuri kwa kuwa alianza kuichezea mechi yake ya kwanza akapata  kadi nyekundu dhidi ya Torino pia majeraha yalikuwa yakimuandama sana na mwezi Agosti mwaka jana alipatwa na maumivu makali sana. 

Pamoja na kutokuwa na maisha mema Inter msimu uliopita, Nemanja aliichezea timu hiyo mechi  23 na kuifungia bao moja.

CHELSEA YAMUWEKA HUYU KATIKA RADA 
Baada ya kumtimua Jose Mourinho kocha aliyechukua mikoba hiyo, Guus Hiddink amekua  akihaha kutafuta watu wa kuimarisha kikosi hicho ili kurudisha hadhi ya timu.

Katika mchakato huo Chelsea wameangukia kwa mshambuliaji  wa PSG Ezequel  Lavezzi mwenye umri wa miaka 30 raia wa Argentina.


Hata hivyo Chelsea itapata wakati mgumu kumpata mchezaji huyo aliyebakiza miezi 6 katika mkataba wake na  kwa mujibu wa  Allesandro Moggi ambaye ni  wakala wake amesema Inter  na Barcelona wanamtaka ila Inter ndo wameonyesha nia ya dhati.

KLOPP HALALI ANAMTAKA HUYU  
Katika kutaka kujiimarisha zaidi, kocha wa Liverpool,  Jurgen Klopp ameamua kuanza biashara na Schalke 04 ya Ujerumani juu  uwezekano wa kumpata Joel Matip.


Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 24 anaweza kupatikana kirahisi kwavile katika mkataba wake amebakiza miezi 6  na hivyo kuwa rahisi kwa  Schalke  kumruhusu mcameroon huyo kwenda kwa majogoo hao wa  Anfield.

Post a Comment

 
Top