BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
1.TONI KROOS 'Profesa'
Huyu ni kiungo kutoka Ujerumani ambaye alishinda tuzo ya kiungo mchezeshaji bora kutoka IFFHS, pia mwaka huo huo alitwaa ubingwa wa dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ujerumani.


Alipewa jina la Profesa na kocha wa wakati huo Carlo Ancelotti kwa kumsifia kiungo huyo katika kufanya maamuzi akiwa na mpira uwanjani, hakika uwezo wake wa utoaji mpira na kusoma mchezo ni wa hali ya juu ndio maana aliitwa Profesa

2.CHRISTIAN VIERI 'Bobo'
Mmoja wa washambuliaji bora waliowahi kutokea katika ligi ya Italia aliechezea klabu 13 katika kipindi cha miaka 18 ya maisha yake ya soka.
Alipewa jina hilo la Bobo kutokana na baba yake aliekuwa mchezaji mpira naye kuitwa Bobo alipokua akicheza huko Australia.

3.FERNANDO TORRES 'El Nino'
Nani asiyemtambua mshambuliaji wa kihispania aliefunga goli pekee katika Euro 2008, Torres alikuwa mshambuliaji hatari aliyeichezea Liverpool akitokea Athletico Madrid klabu ya utoto wake.


Alipokua Athletico aliweza kucheza kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 16 na kwa vile mashabiki hawakuwa wakimtambua kama mastaa waliokuwepo apo ikabidi wamuite El nino wakimaanisha 'mtoto'. Ingawa umri unaenda Torres sura yake hakika inafanana sana na alivyokuwa mtoto.

4.SERGIO AGUERO 'El Kun'
 Huyu ni mshambuliaji hatari katika ligi ya Uingereza raia wa Argentina anayesifika kwa uwezo wa kupachika magoli, njia aliyopata jina lake la utani inastaajabisha kwani alielezea kuwa akiwa mdogo alikuwa anaangalia katuni ambayo kinara wa katuni iyo aliitwa Kum Kum, babu yake alianza kumuita Ko, baadae akamuita Kum na mwisho ndio akalibadili na kumuita Kun na likabaki hivyo hadi leo hii anatambulika kama Kun Aguero


5. FRANK RIBERY 'Scarface'
Winga huyo wa Bayern Munich ni mmoja ya watu walio na bahati sana. Akiwa na umri wa miaka miwili, familia yake ilipata ajali mbaya. Ingawa hakupoteza maisha katika ajali hiyo, alipatwa na jeraha kubwa usoni mwake ambalo hadi leo hii limeacha kovu kubwa.


Alipewa jina hilo katika utoto wake na alipata wakati mgumu ila hakukata tamaa katika ndoto yake ya kuja kuwa mchezaji mahiri duniani

6. WALTER PANDIANI 'Rifle'
Mchezaji huyu anaweza kuwa si mshambuliaji bora sana aliyewahi kutokea nchini Argentina ila alikuwa mshambuliaji aliyesumbua sana mabeki, jina hilo la Rifle lilitokana na uwezo wake wa kuwatungua makipa. Unaweza usimkumbuke Pandiani ila Ac Milan daima watamkumbuka.

7. LIONEL MESSI 'La Pulga'
Hata umpende vipi Cristiano Ronaldo ila lazima utakubaliana na uwezo wa mchezaji bora wa dunia ambaye jana alinyakua tuzo yake ya tano. Alipewa jina la La Pulga likimaanisha kiroboto kutokana na umbo lake lilivyokuwa wakati akiwa mtoto. Lilikuwa dogo ndipo akawa anafananishwa na mdudu huyo mdogo sana.8. STUART PIERCE 'Psycho'
Hili laweza kuwa jina linalochekesha katika haya 10 kwani humaanisha chizi. Pierce ambaye alikua beki bora zaidi kwenye miaka ya 90, alipachikwa jina hilo alipojiunga na klabu ya Nottigham Forest mwaka 1985.

Alipewa jina hilo la Chizi kutokana na tabia yake ya kupiga kelele sana uwanjani huku akisifika kwa kuwavaa vibaya washambuliaji wa timu pinzani wakiwa uwanjani.

9.ARJEN ROBBEN 'The Flying Dutchman'
Huwezi ukacheza Real Madrid, Bayern Munich na Chelsea bila ya kuwa na kipaji cha hali ya juu. Winga huyu anasifika kwa kasi yake akiwa na mpira na anavyowasumbua mabeki wa timu pinzani.
Kasi na tabia yake ya kujidondosha sana ndio iliyompatia jina la utani 'mpaaji wa kiholanzi'


10.ROBERTO BAGGIO  'The Divine Ponytail'
Huyu ni mmoja wa washambuliaji mahiri wa Italia, alishinda tuzo ya mchezaji bora 1993. Alipata jina hilo la The Divine Ponytail kutokana na staili yake ya nywele na imani yake ya Kibuddha.

Post a Comment

 
Top