BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Abra David, Kwa Msaada Wa Mitandao
1. WILLIAM GALLAS (Arsenal Kwenda Chelsea)
Beki huyu raia wa ufaransa aliyekuwa kisiki katika kipindi chake, baada ya kuitumikia klabu yake ya Chelsea kwa miaka mitano alikataa kusaini mkataba mpya klabuni hapo kwa madai kuwa hakupewa fedha anayostahili.

Gallas aliwastaajabisha watu pale aliposema kama hatoruhusiwa aondoke basi atajifunga magoli hapo ndipo alipoondoka na kuhamia kwa mahasimu wao wa London, Arsenal.


2. CESC FABREGAS (Arsenal Kwenda Chelsea)
Raia huyu wa Hispania ambaye ni kiungo aliyesifika kwa kupiga pasi za mwisho akiwa klabuni Arsenal, aliiacha timu hiyo na kuelekea Barcelona.  Msimu wake wa pili katika klabu hiyo haukua mzuri hivyo kumfanya ahamie Chelsea klabu ambayo mwaka 2014 akiwa Arsenal, aliapa kutovaa jezi yake.

Fabregas amefanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza akiwa na Chelsea na sasa ni mchezaji muhimu klabuni hapo.


3. MARIO GOTZE (Borussia Dortmund kwenda Bayern Munich)
Mario Gotze alihama klabu ya utoto wake na aipendayo Borussia Dortmund na kuamua kwenda kwa mahasimu wao wakubwa Bayern Munich.Imekuwa ikiaminika kuwa Mario Gotze alienda Bayern kwa kufuata maslahi mazuri zaidi.


4. CARLOS TEVEZ (Manchester United kwenda Manchester City)
Mshambuliaji huyu raia wa Argentina amehama klabu nyingi ila uhamisho wake ndani ya jiji la Manchester ndio ulikuwa gumzo.Mchezaji huyo alifanya vyema akiwa United huku akiisaidia timu hiyo kutwaa taji la klabu Bingwa Ulaya na ubingwa wa ligi ya Uingereza kabla hajahamia upande wa pili kwa mahasimu wao.5. ROBIN VAN PERSIE (Arsenal kwenda Manchester United)
Mshambuliaji huyu wa kidachi aliondoka Arsenal na kwenda Man United akiwa mchezaji tegemeo. Hali hii ilipelekea mashabiki wa Arsenal wamchukie kwavile klabu bado ilikuwa ikihitaji sana huduma yake.

Van Persie aliitumikia klabu ya Arsenal kwa miaka minane alipofika United alifanikiwa kutwaa taji la ligi kuu akiwa na klabu hiyo.


6. EMMANUEL ADEBAYOR (Arsenal kwenda Tottenham Hotspurs)
Hakika ni maamuzi magumu kutoka timu moja kwenda timu nyingine tena ambayo ni hasimu mkubwa wa timu utokayo. Kwa wenzetu ni usaliti mkubwa kwa klabu.

Emanuel Adebayor baada ya kuhamia Tottenham aliwachefua mashabiki wa Arsenal pale alipofunga bao na kushangilia mbele yao. Hiyo ilichukuliwa kuwa ni dhihaka na usaliti mkubwa kwa  klabu yake ya zamani.


7. ZLATAN IBRAHIMOVIC (Inter Milan Kwenda AC Milan)
Inter Milan na AC Milan ni klabu hasimu ambazo zinatumia uwanja mmoja wa San SiroUhasama kati ya klabu hizi ni mkubwa lakini ulimwengu haukuamini pale nyota wa Inter Milan, Zlatan Ibrahimovic alipohamia AC Milan. 


8. SOL CAMBELL (Tottenham Hotspurs Kwenda Arsenal)
Beki wa zamani wa kimataifa raia wa Uingereza aliweza kuwasaliti Spurs na kujiunga na washika bunduki wa London, Arsenal kwa lengo la kwenda kupata mafanikio zaidi ya kisoka.

Mashabiki wa spurs walilaumu sana kitendo hicho na kuamua kumpachika jina ya Yuda.


9. LUIS FIGO (Barcelona kwenda Real Madrid)
Luis Figo alikuwa mchezaji bora katika idara yake ya ushambuliaji wa pembeni, katika miaka mitano aliyokuwa Barcelona alipata mafanikio makubwa lakini bado aliwakimbia na kuhamia kwa mahasimu wao wakubwa, Real Madrid.Tangu ajiunge na Madrid, alikuwa akipewa wakati mgumu sana mashabiki wa Barca pale timu hizo zilipokutana. Mara kadhaa walimtupia vitu mbalimbali kwa kuonesha hisia zao za chuki juu ya usaliti huo.


10. ASHLEY COLE (Arsenal kwenda Chelsea)
Beki bora wa kushoto wa kiingereza alicheza kwa kiwango cha juu sana akiwa anachipukia hadi anakomaa akiwa Arsenal. Hakutosheka na mshahara aliolipwa Arsenal  akaona aende kwa mahasimu wao wa London Chelsea, ili kipato kiongezeke. Alifanikiwa kujiunga na Chelsea ambapo aliweza kutwaa Ubingwa wa Klabu barani Ulaya na ubingwa wa ligi na ule wa shirikisho la soka la nchini Uingereza, FA.

Post a Comment

 
Top