BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu Kwa Msaada Wa Mitandao

MPIRA wa miguu ndio mchezo ambao umesambaa na kupendwa zaidi duniani kote. Watu wa jinsia, rika na hadhi mbalimbali wamekuwa mashabiki wakubwa wa mchezo huu. Hawa hapa ni watu 10 maarufu na timu zao za soka wanazoshabikia

1.RAFAEL NADAL - Real Madrid
Huyu ni mchezaji bora wa Tenisi ambaye ameshinda mataji makubwa yote katika mchezo huo. Hawezi kuzuia hisia zake linapokuja suala la soka, ni shabiki mkubwa wa Real Madrid ya Hispania na amekuwa pia akijihusisha na kupendekeza wachezaji gani wasajiliwe katika klabu hiyo anayoihusudu. Mara kadhaa Nadal amekuwa akionekana uwanjani kuipa sapoti timu yake hasa inapocheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Santiago Bernabeu.


2.KOBE BRYANT - Barcelona
Staa huyu wa mpira wa kikapu aliyeichezea klabu ya LA Lakers kwa mafanikio makubwa na  kuipatia ubingwa wa Ligi ya kikapu huko Marekani, ni shabiki wa kutupwa wa wakatalunya hao.Mara kwa mara amekuwa akionyesha mapenzi yake kwa kuvaa jezi za Barcelona na kupiga picha.


3.MEEK MILL - Arsenal
Mill ni rapa anayekuja kwa kasi sana katika mziki huko Marekani na duniani kiujumla. Amekuwa shabiki wa Arsenal ya England kwa muda mrefu.

Imefikia hatua mwanamuziki huyu anapanda jukwaani akiwa amevaa jezi ya washika bunduki hao na kufanya maonyesho yake.


4.ELTON JOHN - Watford
Nani asiyemjua mwanamuziki huyu nguli aliyetamba na vibao kama 'Candle in the wind', 'sacrifice' na vingine vingi?.
Basi huyu ni mmoja kati ya mashabiki wakubwa wa Watford timu ambayo kwa sasa inaongozwa vema na Sanchez Flores.


5.DAVID CRAIG - Liverpool
Kwa wale wapenzi wa filamu basi Mr Bond mpya baada ya Pierce Bosnan ni huyu David Craig anayebamba na kukonga nyoyo za mashabiki wake. Nyota huyu anayetamba na filamu ya mwisho ya Bond inayoitwa Spectre, amekuwa akionekana mara kwa mara akiangalia timu yake kipenzi ikicheza pale Anfield.


6.WILL FERRELL - Chelsea

Huyu pia ni nyota wa filamu ila yeye hujulikana zaidi kwa vituko vya kuvunja mbavu. Filamu ya mwisho alicheza na Kevin Hard Get Hard.

Hakika inachekesha sana. Akitoka kwenye majukumu yake basi hafichi mapenzi yake kwa The Blues yenye makazi yake jijini London.


7.DAVID CAMERON - Aston Villa
Pengine unaweza kudhani viongozi wa siasa wapo mbali na michezo ila licha ya Prince Williams, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ni shabiki mkubwa sana wa Aston Villa inayofahamika kwa jina la utani la Villains.


8.USAIN BOLT - Manchester United
Huyu ni mwanariadha mahiri aliyeweka rekodi ya Dunia ya kukimbia mita 100 kwa sekunde 9 tu, hakika dunia inatambua uwezo wake mkubwa katika riadha.Lakini pia katika ushabiki wa Soka mfukuza upepo huyu ni mnazi wa Mashetani Wekundu wa Old Trafford. Kuna wakati ambao ilifikia hatua ya kuhusishwa na kutaka kufanyiwa majaribio katika klabu hiyo ambayo ipo moyoni mwake.


9.HUGH JACKMAN - Norwich City

Unamkumbuka Wolverine katika filamu ya Xmen?. Basi ndo huyu Jackman ambaye humwambii chochote kuhusu chama lake Norwich City.
10.DANIEL RADCLIFFE - Fulham
Unaweza kudhani Fulham ni klabu ndogo ila masupastaa kibao wanaishabikia.

Mmoja wao ambaye ni marufu zaidi ni huyu Daniel ambaye alibamba katika Harrypotter. Huyu alianza kuipenda klabu hiyo tangu akiwa mdogo akianza kufatilia mpira wa miguu.

Post a Comment

 
Top